EXHIBITS
Mradi wa Usambara: Mandhari ya Mabadiliko na Endalevu katika Milima Usambara ya Mashariki, c. 1910: Shamba la Kwai na Bonde, c. 1914 na 2016
English
Shamba la Kwai
Shamba la Kwai na Bonde, c. 1914
Dobbertin alipiga picha hii kutoka mbali zaidi na kuonyesha ghala, machinjio, na bonde la juu. Picha hiyo inaangazia kampeni za upandaji miti zilizoendelea katika maeneo haya. Wafanyakazi wa Eick walipanda miti ya mikaratusi (Eucalyptus) juu ya nyumba na kuweka katika bustani kubwa ya mimea ya majaribio huko Kwai na Mkuzi jirani. Pia walichunga ng’ombe kwenye malisho ambayo wafugaji wa kimbugu walikuwa wametengeneza katika mabonde yote mawili.
Tangu awali, mradi wa Ujerumani ulikuza chuki kali kati ya wa mbugu wanaoishi karibu na mipaka ya mali isiyohamishika. Viongozi wa walisafiri hadi makao makuu ya mkoa wa Tanga kutoa malalamiko yao dhidi ya Eick na mamlaka ya Wilaya ya Lushoto. Mnamo 1902, Ludwig Illich alichukua ukodishaji wa mali isiyohamishika na kupanua uendeshaji wa mifugo, akiongeza majengo katikati ya picha. Historia ya vurugu ya Kwai inaunda mitazamo wa sasa kuihusu. Bila shaka, watu wa kabila la wa Mbugu waliounda mazingira ya thamani waliomboleza hasara yake. Urithi wa Kwai wa vurugu ni pamoja na kupigwa kwa umma, kufanya kazi kwa lazima {utumwa}, kupigwa risasi na polisi, kuchomewa nyumba, na mauaji.
Shamba la Kwai na Bonde, Picha ya marudio, 2016
Prof. Conte hakuweza kufikia sehemu ya juu ya kilima cha Dobbertin, lakini tovuti ya kurudia picha iko karibu. Mabadiliko ni makubwa. Sehemu za mikaratusi zimetoweka, ingawa Prof. Conte alitembelea mikaratusi michache mwaka wa 1998. Bonde hili sasa ni bustani badala ya malisho. Msitu kwenye miteremko ya juu juu ya shamba umetoweka. Hatimaye, watu wameondoa majengo ya kijerumani. Picha inaonyesha bonde lililogawanywa kati ya watu wengi ingawa kuna nyumba chache kwenye uwanja wa mali. Juu ya sakafu ya bonde, wakulima wamepanda miti muhimu kama vile misaji (grevillia) kwa yambao na kuni pamoja na parachichi matunda ya kuuza sokoni. Kabichi hukua vizuri hapa kama vile mazao mengine ya sokoni kama vile karoti na viazi. Kilimo kichanga cha misonobari hukua miguuni mwa Prof. Conte. Hali ya hewa ya joto sasa inaruhusu ndizi kukua sasa Kwai, jambo lisilowezekana katika miaka ya 1910. Kwa hakika watu wanajua kuhusu maisha ya vurugu ya Kwai na wanajilinda dhidi ya hisia hasi kwa kutumia fingo, ambazo Prof. Conte alizipata zikining'inia kutoka kwa miti michache ya parachichi.